ص
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
أَتَّخَذْنَـٰهُمْ سِخْرِيًّا أَمْ زَاغَتْ عَنْهُمُ ٱلْأَبْصَـٰرُ ٦٣
{63} "Tulikosea tulipowafanyia masihara, au macho yetu tu hayawaoni?" Yaani kutowaona kwetu kunatokana na mambo mawili: ima tulikosea katika kuwazingatia kwamba ni waovu, ilhali kwa hakika wao ni miongoni mwa wema, lakini tukawaita hivyo tu kwa njia ya kuwakejeli. Na huu ndio ukweli, kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema kuhusu watu wa Motoni: "Bila ya shaka lilikuwepo kundi katika waja wangu likisema: Mola wetu Mlezi! Tumeamini, basi tusamehe na uturehemu, nawe ndiwe Mbora wa wanaorehemu. Lakini nyinyi mliwakejeli hata wakakusahaulisheni kunikumbuka, na mlikuwa mkiwacheka." Jambo la pili ni kwamba pengine macho yetu yamekengeuka na hatuwezi kuwaona pamoja nasi Motoni. Vinginevyo, wanapaswa kuwa pamoja nasi wakiadhibiwa, lakini ni macho yetu ambayo hayawaoni. Inawezekana kwamba hayo ndiyo yaliyomo katika nyoyo zao. Kwa hivyo itikadi hiyo waliyoiitakidi duniani na wakawahukumu waumini kwamba wataingia Motoni, ilibakia madhubuti katika mioyo yao na ikawa ndiyo rangi yake. Basi wakaingia Motoni wakiwa katika hali hii, ndiyo maana wakasema hayo waliyosema. Na inawezekana kwamba maneno yao haya ni ya kuficha haki, kama walivyoificha duniani. Na ndiyo maana watu wa Al-A`raf wakawaambia watu wa Motoni: "Je, hawa sio wale mliokuwa mkiwaapia kuwa Mwenyezi Mungu hatawafikishia rehema? Ingieni Peponi, hapana khofu kwenu, wala hamtahuzunika!"