ص
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَعَجِبُوٓا۟ أَن جَآءَهُم مُّنذِرٌ مِّنْهُمْ ۖ وَقَالَ ٱلْكَـٰفِرُونَ هَـٰذَا سَـٰحِرٌ كَذَّابٌ ٤
{4} "Na walistaajabu kuwajia mwonyaji anayetokana nao wenyewe." Yaani, hao wanaokadhibisha walistaajabia jambo ambalo sio la kustaajabisha, kwamba aliwajia mwonyaji anayetokana nao wenyewe ili wapate kujifunza kutoka kwake na kumjua vyema zaidi; na kwa kuwa yeye ni miongoni mwa watu wao ili wasione ugumu wa kufuata mtu asiyekuwa wa kutokana nao. Kwani walipaswa kushukuru na kumtii kikamilifu kwa sababu ya hili, lakini wao walifanya kinyume cha jambo hili na wakastaajabia kwa njia ya kukanusha. Na kwa sababu ya ukafiri wao na dhuluma yao wakasema: "Huyu ni mchawi, mwongo mno."