ص
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَهَلْ أَتَىٰكَ نَبَؤُا۟ ٱلْخَصْمِ إِذْ تَسَوَّرُوا۟ ٱلْمِحْرَابَ ٢١
{21} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja kwamba alimpa Nabii wake Daudi uwezo wa kukata hukumu sawasawa baina ya watu, na ilikuwa akijulikana kwa hilo na watu wakawa wanamjia kwa ajili yake. Mwenyezi Mungu akataja habari za wapinzani wawili waliogombana mbele yake kwa sababu ya jambo fulani, na Mwenyezi Mungu aliwafanya kuwa ni mtihani kwa Daudi na mawaidha kwa sababu ya kosa alilokuwa amelifanya. Basi Mwenyezi Mungu akamsamehe na akamuwekea tukio hili. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akamwambia Nabii wake Muhammad - rehema na amani zimshukie: "Na je, imekufikia habari ya wagombanao?" Kwani ni habari za ajabu "walipopindukia ukuta kuingia chumbani" mwa Daudi mwa kuabudia bila ya ruhusa yoyote, na wala hawakuingilia mlangoni.