انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · ص
السورة ٣٨

ص

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٧

ٱصْبِرْ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَٱذْكُرْ عَبْدَنَا دَاوُۥدَ ذَا ٱلْأَيْدِ ۖ إِنَّهُۥٓ أَوَّابٌ ١٧

{17} Basi Mwenyezi Mungu akamwambia Mtume wake: "Subiri kwa wanayoyasema" kama walivyosubiri Mitume kabla yako. Maneno yao hayadhuru haki kwa vyovyote vile, wala hawakudhuru chochote, bali wanajidhuru tu.

{17} Mwenyezi Mungu alipomwamrisha Mtume wake kuwa na subira juu ya kaumu yake, akamuamrisha atafute msaada wa kuwa na subira hiyo kwa kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake. Na kwamba akumbuke hali ya watu waliokuwa wakimuabudu Mwenyezi Mungu sana. Kama alivyosema katika aya nyingine: "Basi yavumilie haya wayasemayo, na umtakase Mola wako Mlezi kwa kumsifu kabla ya kuchomoza jua na kabla halijachwa." Miongoni mwa wale waliokuwa wakimuabudu Mwenyezi Mungu sana ni Nabii wa Mwenyezi Mungu, Daudi, rehema na amani ziwe juu yake. Ambaye alikuwa "mwenye nguvu" nyingi katika kumwabudu Mwenyezi Mungu katika mwili wake na moyo wake. "Hakika yeye alikuwa mwingi wa kutubia" kwa upendo, kumfanyia uungu, hofu, matumaini, kuomba dua nyingi kwa unyenyekevu na kurudi kwake pale anapokosea kwa kuachana na kosa hilo na kutubia toba ya kweli.