ص
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
صٓ ۚ وَٱلْقُرْءَانِ ذِى ٱلذِّكْرِ ١
{1} Huku ni kubainisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kuhusu hali ya Qur-ani na hali ya wale wanaoikadhibisha, namna wanavyoamiliana nayo na pia namna wanavyoamiliana na yule aliyekuja nayo. Akasema: "Swad. Ninaapa kwa Qur-ani yenye mawaidha," cheo kikuu na utukufu. Ambayo huwakumbusha waja kila wanachohitaji miongoni mwa elimu ya majina ya Mwenyezi Mungu, sifa zake, na vitendo vyake. Na pia elimu ya hukumu za Mwenyezi Mungu. Na pia elimu kuhusu akhera na hukumu za kimalipo. Inakumbusha mambo ya kimsingi na ya matawi ya dini yao. Hapa hakuna haja ya kumtaja yule ambaye imeapwa kwa ajili yake. Kwani uhakika wa hilo hapa ni kwamba kilichoapiwa na kilichoapwa kwa ajili yake ni kitu kimoja, nacho ni Qur-ani hii, yenye maelezo haya matukufu.