الصافات
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَبَـٰرَكْنَا عَلَيْهِ وَعَلَىٰٓ إِسْحَـٰقَ ۚ وَمِن ذُرِّيَّتِهِمَا مُحْسِنٌ وَظَالِمٌ لِّنَفْسِهِۦ مُبِينٌ ١١٣
{113} "Tukambarikia yeye na Is-haqa" katika elimu yao, matendo yao na vizazi vyao. Basi Mwenyezi Mungu akaeneza mataifa matatu makubwa kutokana na dhuria zao: Waarabu kutokana na dhuria ya Ismail, Wana wa Israeli na taifa la Kirumi kutokana na kizazi cha Is-haq. "Na miongoni mwa dhuria zao walitokea wema na wenye kudhulumu nafsi zao waziwazi." Yaani, miongoni mwao wapo wema na wabaya, waadilifu na madhalimu, ambao dhuluma yao imedhihirika kwa ukafiri wao na ushirikina wao. Na pengine hii ni kwa ajili ya kuondoa dhana mbaya aliposema: "Tukambarikia yeye na Is-haqa." Kwamba hilo linamaanisha kwamba vizazi vyao pia vimebarikiwa na kwamba wao wote ni watu wema. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akatujulisha kwamba miongoni mwao wapo watenda mema na madhalimu. Na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi.