الصافات
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
فَلَمَّا بَلَغَ مَعَهُ ٱلسَّعْىَ قَالَ يَـٰبُنَىَّ إِنِّىٓ أَرَىٰ فِى ٱلْمَنَامِ أَنِّىٓ أَذْبَحُكَ فَٱنظُرْ مَاذَا تَرَىٰ ۚ قَالَ يَـٰٓأَبَتِ ٱفْعَلْ مَا تُؤْمَرُ ۖ سَتَجِدُنِىٓ إِن شَآءَ ٱللَّهُ مِنَ ٱلصَّـٰبِرِينَ ١٠٢
{102} "Basi alipofika makamo ya kwenda na kurudi pamoja naye," katika umri ambao kwa kawaida huwa anapendeza zaidi kwa wazazi wake, ambapo ugumu wa kumlea huwa umepunguka na manufaa yake yakaanza kutokea, basi Ibrahim, amani iwe juu yake, akamwambia: "Hakika mimi nimeona usingizini kuwa ninakuchinja," kwa amri ya Mwenyezi Mungu. Na ndoto za Manabii ni ufunuo. Basi angalia wewe, waonaje?" Kwa maana amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ni lazima itekelezwe. Kwa hivyo Ismail akasema kwa uvumilivu na kutumaini malipo ya Mwenyezi Mungu, huku amemridhia Mola wake Mlezi na kumfanyia wema baba yake: "Ewe baba yangu! Tenda unavyoamrishwa, utanikuta mimi, Inshallah Mwenyezi Mungu akipenda), katika wanaosubiri." Kwa sababu hakuna kinachotokea bila mapenzi ya Mwenyezi Mungu.