انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · يس
السورة ٣٦

يس

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٨٣

فَسُبْحَـٰنَ ٱلَّذِى بِيَدِهِۦ مَلَكُوتُ كُلِّ شَىْءٍ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ٨٣

{83} "Basi ametakasika yule ambaye mkononi mwake umo Ufalme wa kila kitu." Huu ni ushahidi wa sita. Kwani Mwenyezi Mungu ndiye Mfalme anayemiliki kila kitu, ambaye vyote vilivyomo katika ulimwengu wa juu na wa chini ni mali yake na waja waliotiishwa na wanaoendeshwa, anawaendesha kwa mipango yake ya kimajaliwa, hukumu zake za kisheria, na hukumu zake za kimalipo. Basi kuwarudisha baada ya kufa kwao ili awatekelezee malipo ni katika ukamilifu wa ufalme wake. Na ndiyo maana akasema: "Na kwake Yeye mtarejeshwa." Na hilo halina shaka yoyote, kwa sababu kuna hoja mbalimbali za uhakika na ushahidi unaong'aa juu yake. Basi ametakasika yule ambaye aliweka katika maneno yake mwongozo, uponyaji na nuru.

Imekamilika tafsiri ya Surat Yasin Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu kama unavyostahiki utukufu wake, ukamilifu wake, ukuu wake na ukubwa wake. Na rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya Mtume wetu Muhammad.