يس
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
ٱتَّبِعُوا۟ مَن لَّا يَسْـَٔلُكُمْ أَجْرًا وَهُم مُّهْتَدُونَ ٢١
{21} Kisha akataja kinachounga mkono yale aliyoyashuhudia na kuyalingania, akasema: "Wafuateni ambao hawakutakini ujira." Yaani, wafuateni wale waliokunasihini kwa njia ambayo itakuleteeni heri, na wala hawataki mali zenu wala malipo yoyote kwa nasaha yao waliyowapa wala kuwaelekeza kwao walikowaelekeza. Haya yanalazimu kwamba afuatwe mtu ambaye hizi ndizo sifa zake. Inabakia kusema: Labda analingania bila ya kuomba ujira, lakini hayuko kwenye haki. Basi akazuia hili kwa kauli yake: "Hali ya kuwa wenyewe wameongoka." Kwa sababu hawalinganii isipokuwa kwenye yale ambayo akili timamu inashuhudia uzuri wake, na wala hawakatazi isipokuwa yale ambayo akili timamu inashuhudia kwamba ni mabaya.