انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · يس
السورة ٣٦

يس

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٨

قَالُوٓا۟ إِنَّا تَطَيَّرْنَا بِكُمْ ۖ لَئِن لَّمْ تَنتَهُوا۟ لَنَرْجُمَنَّكُمْ وَلَيَمَسَّنَّكُم مِّنَّا عَذَابٌ أَلِيمٌ ١٨

18. Basi watu wa kijiji hicho wakawaambia Mitume wao: "Sisi tumeamua kuwa nyinyi ni wakorofi." Yaani, hatukuona katika kutujia kwenu na kuingiliana kwenu nasi isipokuwa uovu tu. Lakini hili ni katika maajabu makubwa zaidi ya yote. Kwamba walimfanya yule aliyewajia na neema kubwa zaidi ambayo Mwenyezi Mungu aliwaneemesha kwayo waja wake, na utukufu mkubwa zaidi aliowakirimu kwa huo, na haja yao juu ya hilo iliyokuwa kubwa zaidi ya mahitaji mengine yote, kwamba alikuja na hali ya uovu ambayo iliwazidishia uovu waliokuwa nao, na wakaona mkosi ndani yake. Lakini huko ni kuachiliwa mbali na Mwenyezi Mungu na kutowezeshwa kunaweza kumfanya mtu huyo mambo makubwa zaidi ya anavyoweza kufanyiwa na adui yake. Kisha wakawatishia wakisema: "Ikiwa hamtaacha basi kwa yakini tutakupigeni mawe." Yaani, tutawauwa kwa kuwapiga mawe vibaya kabisa. "Na mtapata adhabu chungu kutoka kwetu."