فاطر
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَهُمْ يَصْطَرِخُونَ فِيهَا رَبَّنَآ أَخْرِجْنَا نَعْمَلْ صَـٰلِحًا غَيْرَ ٱلَّذِى كُنَّا نَعْمَلُ ۚ أَوَلَمْ نُعَمِّرْكُم مَّا يَتَذَكَّرُ فِيهِ مَن تَذَكَّرَ وَجَآءَكُمُ ٱلنَّذِيرُ ۖ فَذُوقُوا۟ فَمَا لِلظَّـٰلِمِينَ مِن نَّصِيرٍ ٣٧
{37} "Na humo watapiga makelele" wakiomba msaada wakisema: 'Mola wetu Mlezi! Tutoe tufanye mema sio yale tuliyokuwa tukiyafanya.'" Basi wakakiri dhambi zao, na wakajua kwamba Mwenyezi Mungu amewafanyia uadilifu, lakini wakaomba kurudi katika wakati usiofaa. Kwa hivyo, wakaambiwa: "Kwani hatukukupeni umri wa kutosha kukumbuka mwenye kukumbuka?" Na akaweze kufanya matendo mema; kwani tuliwastarehesha duniani na tukawapa riziki kwa wingi, na tukawaongezea muda wa kuishi, na tukawatumia Ishara kwa kufuatanisha, na pia tukawafikishia waonyaji, na tukawajaribu kwa mema na dhiki, ili mtubu na mrejee kwetu. Lakini maonyo hayo hayakuwaingia, wala mawaidha hayakuwanufaisha, na tukawacheleweshea adhabu itokayo kwenu, mpaka ulipokwisha muda wenu na mkaondoka katika makao ya uwezekano katika hali mbaya zaidi na mkaifikia nyumba hii ya malipo kwa matendo; mkaomba kurudi! Hapana, hapana! Wakati wa kuwezekana umeshapita, na ameshawakasirikia Mwingi wa kurehemu, Mwingi wa rehema, na adhabu ya Moto imekuwa kali kwenu, na wakazi wa Peponi wameshawasahau. Basi kaeni humo milele na milele katika adhabu mkifedheheshwa. Na ndiyo maana akasema: "Basi onjeni! Kwani wale waliodhulumu hawana wa kuwanusuru," atakayewanusuru na kuwaondoa humo au atakayewapunguzia adhabu yake.