فاطر
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
إِن تَدْعُوهُمْ لَا يَسْمَعُوا۟ دُعَآءَكُمْ وَلَوْ سَمِعُوا۟ مَا ٱسْتَجَابُوا۟ لَكُمْ ۖ وَيَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ يَكْفُرُونَ بِشِرْكِكُمْ ۚ وَلَا يُنَبِّئُكَ مِثْلُ خَبِيرٍ ١٤
{14} Na pamoja na haya: "Ukiwaomba" hawatawasikia; kwa sababu wao wako baina ya vitu visivyo na uhai, wafu. Na Malaika ambao wanajishughulisha na kumtii Mola wao Mlezi, "na hata wakisikia" kama itachukuliwa hivyo "hawakujibuni." Kwa sababu wao hawamiliki chochote na wengi wao hawaridhiki na ibaada za wale wanaowaabudu. Na ndiyo maana akasema: "Na Siku ya Kiyama watakataa ushirikina wenu." Yaani, watajitenga mbali nanyi, na watasema: Umetakasika, wewe ndiye mlinzi wetu si wao. "Na hapana atakayekupa habari vilivyo kama Yeye Mwenye habari." Yaani, hakuna anayekupa habari kwa ukweli zaidi kuliko Mwenyezi Mungu, Mjuzi wa yote, Mwenye habari zote. Basi kuwa na uhakika kwamba jambo hili ni kama kwamba ni jambo linaloonwa kwa jicho, basi huwezi kuwa na shaka nalo na kusitasita. Aya hizi zinajumuisha ushahidi wazi na hoja za kung'aa zinazoonyesha kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye Mwenye kufanyiwa uungu na kuabudiwa peke yake. Na ambaye hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Yeye, na kwamba kuabudu asiyekuwa Yeye ni batili, na kuabudu huko kunahusiana na batili ambayo haifai kitu mwenye kuiabudu.