انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · فاطر
السورة ٣٥

فاطر

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٢

وَمَا يَسْتَوِى ٱلْبَحْرَانِ هَـٰذَا عَذْبٌ فُرَاتٌ سَآئِغٌ شَرَابُهُۥ وَهَـٰذَا مِلْحٌ أُجَاجٌ ۖ وَمِن كُلٍّ تَأْكُلُونَ لَحْمًا طَرِيًّا وَتَسْتَخْرِجُونَ حِلْيَةً تَلْبَسُونَهَا ۖ وَتَرَى ٱلْفُلْكَ فِيهِ مَوَاخِرَ لِتَبْتَغُوا۟ مِن فَضْلِهِۦ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ١٢

{12} Huku ni kujulisha kuhusu uwezo wake, hekima yake na rehema. Kwamba alizifanya bahari mbili kwa ajili ya masilahi ya ulimwengu wote wa dunia, na kwamba hakuzilinganisha, kwa sababu masilahi yanahitaji kwamba mito iwe na maji matamu yenye ladha, mazuri kunywa; ili wafaidike kwayo wanywaji na wakulima, kwamba pia iwe na maji ya chumvi machungu; ili hewa inayoizunguka ardhi isiharibike kwa harufu za wanyama wanaofia baharini, na kwa sababu imetulia na haitiririki. Hii ni kwa sababu kuwa kwake ni chumvi kunaizuia kubadilika, na ili wanyama wake wawe bora na watamu zaidi. Ndiyo maana akasema: "Na kutokana na bahari zote mbili" ya maji ya chumvi na ya maji matamu "mnakula nyama mpya (isiyochacha);" nayo ni samaki anayeweza kuvuliwa katika bahari. Na mnatoa mapambo mnayoyavaa," kama vile lulu na marijani na vitu vinginevyo vinavyopatikana baharini. Haya ni masilahi makubwa kwa watu. Katika masilahi na manufaa mengine katika bahari ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu aliitiisha ili ibebe merikebu na mashua. Basi utaziona zikiikata na kuipasua bahari zikakwenda kutoka eneo moja kwenda eneo jingine na kutoka sehemu moja hadi nyingine, zikiwabeba wasafiri, mizigo yao na biashara zao. Na kutokana na hayo zinapatikana fadhila za Mwenyezi Mungu na wema wake mwingi sana, na ndiyo maana akasema, "ili mtafute fadhila zake, na ili mpate kushukuru."