انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الروم
السورة ٣٠

الروم

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٥٦

وَقَالَ ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْعِلْمَ وَٱلْإِيمَـٰنَ لَقَدْ لَبِثْتُمْ فِى كِتَـٰبِ ٱللَّهِ إِلَىٰ يَوْمِ ٱلْبَعْثِ ۖ فَهَـٰذَا يَوْمُ ٱلْبَعْثِ وَلَـٰكِنَّكُمْ كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ٥٦

{56} "Na wale waliopewa elimu na Imani watasema;" yaani, Mwenyezi Mungu aliwaneemesha mawili hayo na yakawa ndiyo sifa yao: kujua haki na kuwa na imani inayolazimu kuipendelea haki. Na ikiwa wanaijua haki na kuipendelea, basi maneno yao lazima yalingane na hali halisi ya mambo, na inayofailia hali zao. Ndiyo maana wakasema kweli, "Hakika nyinyi mlikwisha kaa katika hukumu ya Mwenyezi Mungu" aliyowaandikia "mpaka Siku ya Kiyama." Yaani, mliishi maisha umri ambao mwenye kukumbuka anakumbuka, na mwenye kuzingatia anazingatia juu yake mpaka ufufuo ulipotokea, na mkafikia hali hii. "Basi hii ndiyo Siku ya kufufuliwa! Lakini nyinyi mlikuwa hamuijui." Ndiyo maana mliikataa duniani, na mkakataa kukaa kwenu duniani kwa muda ambao mngeweza kurudi kwa Mwenyezi Mungu na kutubu. Basi haukuacha ujinga kuwa ndio kauli mbiu yenu, na athari zake kama vile kukadhibisha na hasara vikawa ndiyo nguo yenu ya juu ya mwili.