انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · العنكبوت
السورة ٢٩

العنكبوت

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٦٩

وَٱلَّذِينَ جَـٰهَدُوا۟ فِينَا لَنَهْدِيَنَّهُمْ سُبُلَنَا ۚ وَإِنَّ ٱللَّهَ لَمَعَ ٱلْمُحْسِنِينَ ٦٩

{69} "Na wale wanaofanya juhudi kwa ajili yetu" nao ni wale waliohamia katika njia ya Mwenyezi Mungu, wakapigana na maadui zao, na wakajitahidi kufuata njia zake "Sisi hakika tutawaongoa kwenye njia zetu" zenye kufikisha kwetu, kwa sababu wao ni wazuri. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja na wazuri kwa kuwasaidia, kuwanusuru na kuwaongoa. Hii ilionyesha kwamba watu wanaostahili zaidi kuwa katika usahihi ni watu wa jihadi. Na kwamba mwenye kufanya vizuri yale aliyoamrishwa, Mwenyezi Mungu humsaidia na kumrahisishia njia za uwongofu. Na kwamba mwenye kufanya bidii katika kutafuta elimu ya kisheria, anapata uwongofu na msaada katika kufikia anachotafuta; ambayo ni mambo ya kiungu ambayo si ya kawaida na asiyoyaelewa huyo mwenye kujitahidi, na jambo lake hilo la kutafuta elimu linakuwa rahisi. Kwa maana kutafuta elimu ya kisheria ni katika jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu. Bali ni mojawapo ya zile aina mbili za jihadi, ambazo hawazifanyi isipokuwa viumbe maalumu. Nazo ni jihadi kwa maneno na ulimi dhidi ya makafiri na wanafiki, na jihadi katika kufundisha masuala ya dini, na jihadi juu ya kuzuia pingamizi za wale wanaoihalifu haki, hata kama wao ni Waislamu.

Imekamilika tafsiri ya Surat Al-Ankabut, kwa sababu ya sifa njema za Mwenyezi Mungu na msaada wake.