العنكبوت
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَكَأَيِّن مِّن دَآبَّةٍ لَّا تَحْمِلُ رِزْقَهَا ٱللَّهُ يَرْزُقُهَا وَإِيَّاكُمْ ۚ وَهُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلْعَلِيمُ ٦٠
{60} Yaani, Yeye Muumba, Mtakatifu, Mtukufu, alichukua dhamana ya kuwapa riziki viumbe vyote, wenye nguvu kati yao na wanyonge wao. Kwa hivyo, "ni wanyama wangapi" katika ardhi wenye akili na nguvu dhaifu ambao "hawawezi kujimilikia riziki zao!" Wala hawaweki akiba, na Mwenyezi Mungu anaendelea tu kuwafikishia riziki katika kila wakati alioupanga. "Mwenyezi Mungu anawaruzuku hao na nyinyi pia." Nyinyi nyote mnamtegemea Mwenyezi Mungu, ambaye anawaruzuku, alivyowaumba na kuwaendesha. "Na Yeye ndiye Mwenye kusikia Mwenye kujua zaidi." Hakuna kinachofichikana kwake, wala hakuna kiumbe anayekufa kwa kukosa riziki kwa sababu kimefichikana kwake, kama Mwenyezi Mungu alivyosema, "Na hakuna mnyama yeyote katika ardhi ila riziki yake iko kwa Mwenyezi Mungu. Naye anajua makao yake na mapitio yake. Yote yamo katika Kitabu chenye kubainisha."