انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · العنكبوت
السورة ٢٩

العنكبوت

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٦

وَإِبْرَٰهِيمَ إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِ ٱعْبُدُوا۟ ٱللَّهَ وَٱتَّقُوهُ ۖ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ١٦

{16} Mwenyezi Mungu Mtukufu anataja kwamba alimtuma rafiki yake Ibrahim, amani iwe juu yake, kwa watu wake, akiwalingania kwa Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo akawaambia, "Muabuduni Mwenyezi Mungu." Yaani, mpwekesheni yeye, mfanyieni yeye ikhlasi kwa kumuabudu, na mtii kile alichowaamuru kufanya, "na mcheni Yeye;" asije akawakisirikia nyinyi na kuwaadhibuni, na hiyo ni kwa kuacha kile kinachomkasirisha katika madhambi. "Hiyo" yaani, kumuabudu Mwenyezi Mungu na kumcha, "ndiyo heri yenu." Yeyote anayeacha hilo, na hii ni chini ya kichwa cha kutoa upendeleo kwa kitu ambacho hakina chochote kwa upande mwingine; akiacha kumwabudu Mwenyezi Mungu na kuacha uchamungu wake, hakuna kheri yoyote kwake. Lakini kumuabudu Mwenyezi Mungu na kumcha Yeye ni kheri kwa watu kwa sababu hakuna njia ya kupata hadhi yake katika ulimwengu huu na Akhera isipokuwa kwa njia hiyo. Basi kila wema uliopo katika ulimwengu huu na Akhera; ni moja ya athari za ibada ya Mungu na uchaji wake "ikiwa nyinyi mnajua." Hilo ni; ya kwamba mjue mambo, na muone ni nini cha kwanza na bora zaidi cha kujitolea.