انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · العنكبوت
السورة ٢٩

العنكبوت

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٤

وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوْمِهِۦ فَلَبِثَ فِيهِمْ أَلْفَ سَنَةٍ إِلَّا خَمْسِينَ عَامًا فَأَخَذَهُمُ ٱلطُّوفَانُ وَهُمْ ظَـٰلِمُونَ ١٤

{14} Anaelezea Mwenyezi Mungu Mtukufu juu ya hukumu yake na hekima yake katika adhabu za mataifa yanayokanusha, na kwamba Mwenyezi Mungu alimtumia mja wake na Mtume wale Nuhu, [swala na] amani ziwe juu yake kwa kaumu wake, aliwalingania kwenye tauhidi, kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa ajili ya ibada, na kuwakataza miungu na masanamu, "na akakaa nao" kama Nabii aliyelingania "miaka elfu kasoro miaka hamsini." Hakuacha kuwalingania na hakuacha kuwashauri; aliwalingania usiku na mchana na kwa siri na kwa uwazi, na hawakuongoka na hawakuongozwa, lakini waliendelea na ukafiri wao na uasi wao. Mpaka Nabii wao Nuhu, Rehema na Amani zimshukie, akawaombea, licha ya subira yake kubwa, ustahimilivu na stahamala yake. Basi akasema "Mola wangu Mlezi! Usimwache juu ya ardhi mkazi wake yeyote katika makafiri!" "Basi tufani ikawachukua" kutoka mbinguni kwa wingi na kutiririka kutoka duniani katika dhiki. "Nao ni madhalimu" na wanastahili adhabu.