النمل
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
يَـٰمُوسَىٰٓ إِنَّهُۥٓ أَنَا ٱللَّهُ ٱلْعَزِيزُ ٱلْحَكِيمُ ٩
{9} "Ewe Musa! Hakika Mimi ndiye Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hekima;" yaani, Mwenyezi Mungu alimwambia kwamba yeye ndiye Mwenyezi Mungu anayestahili kuabudiwa peke yake na hana mshirika yeyote; kama ilivyo katika aya nyingine: "Hakika Mimi ndiye Mwenyezi Mungu. Hapana mungu isipokuwa Mimi tu. Basi niabudu Mimi, na ushike Swala kwa ajili ya kunikumbuka Mimi." "Mwenye nguvu," ambaye alishinda vitu vyote na viumbe vyote vilimnyenyekea. "Mwenye hekima" katika amri yake na uumbaji wake, na katika hekima yake ni kwamba alimtuma mja wake Musa bin Imran, ambaye alijua kwamba kupewa utume, na ufunuo na kumuongelesha. Na katika nguvu zake ni kwamba unamtegemea Yeye na wala huwezi kuona upweke unapokuwa peke yako hata kama maadui zako wengi na wenye nguvu nyingi; kwani nywele za mbele ya kichwa chao ziko mikononi mwa mwenyezi Mungu, harakati zao na ukimya wao ni kulingana na uendeshaji wake.