النمل
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَيَوْمَ يُنفَخُ فِى ٱلصُّورِ فَفَزِعَ مَن فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَمَن فِى ٱلْأَرْضِ إِلَّا مَن شَآءَ ٱللَّهُ ۚ وَكُلٌّ أَتَوْهُ دَٰخِرِينَ ٨٧
{87} Mwenyezi Mungu anawaogopesha waja wake yaliyo mbele yao katika Siku ya Kiyama, magumu, dhiki, na mambo yanayosumbua nyoyo yaliyo ndani yake. Akasema, "Na Siku litakapopulizwa baragumu, watahangaika" kwa sababu ya kupulizwa kwake "waliomo mbinguni na katika ardhi," na watachanganyika wao kwa wao kwa sababu ya kuhofu mambo ambayo ni utangulizi wake "isipokuwa amtakaye Mwenyezi Mungu" miongoni mwa wale ambao Mwenyezi Mungu aliwatukuza na akawaimarisha na kuwahifadhi kutokana na mahangaiko hao. "Na" viumbe "wote" wakati litakapopulizwa baragumu, "watamfikia huku ni wanyonge" na wadhalilifu. Kama Mwenyezi Mungu alivyosema, "Hapana yeyote aliyemo mbinguni na ardhini isipokuwa atamjia Arrahmani (Mwingi wa rehema) akiwa mja tu." Katika siku hiyo, wakuu na walio chini yao watakuwa sawa katika kudhalilika na kumnyenyekea Mfalme wa wafalme.