انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النمل
السورة ٢٧

النمل

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٦

وَوَرِثَ سُلَيْمَـٰنُ دَاوُۥدَ ۖ وَقَالَ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ عُلِّمْنَا مَنطِقَ ٱلطَّيْرِ وَأُوتِينَا مِن كُلِّ شَىْءٍ ۖ إِنَّ هَـٰذَا لَهُوَ ٱلْفَضْلُ ٱلْمُبِينُ ١٦

{16} Alipowasifu kwa pamoja, akamtaja Sulemani peke yake kwa sababu ya yale ambayo Mwenyezi mungu alimpa yeye tu; kwani Mwenyezi Mungu alimpa ufalme mkuu na akawa na mambo ambayo baba yake, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, hakuwahi kuwa nayo. Mwenyezi Mungu akasema: "Na Sulaiman alimrithi Daudi' yaani, alirithi katika elimu yake na unabii wake, na elimu ya baba yake ikaungana na elimu yake, kama ilivyotangulia katika kauli yake, "Kwa hivyo tukamfahamisha Suleiman" "na akasema:" akimshukuru Mwenyezi Mungu na kujisifu kwa hisani yake na kuzungumzia neema yake, "Enyi watu! Tumefunzwa usemi wa ndege." Na alikuwa yeye amani iwe juu yake akielewa yale wanayosema; kama alivyozungumza na Hud-Hud, naye Hud-Hud akazungumza naye. Na kama alivyoelewa maneno ya mchwa alipowaongelesha mchwa wenzake, kama itakavyokuja. Na hili halikuwahi kutokea kwa mtu yeyote isipokuwa Sulemani, amani iwe juu yake, "na tumepewa katika kila kitu" yaani: Mwenyezi Mungu alitupa neema na sababu za ufalme na utawala, na ushindi ambao hakuwahi kumpa mwanadamu yeyote. Na ndiyo sababu akamwomba mola wake Mlezi, akasema: "Mola wangu Mlezi! Nisamehe na unipe ufalme usiomwelekea yeyote baada yangu." Kwa hivyo mwenyezi Mungu akamtiishia mashetani wakawa wanamfanyia kila kitu anachotaka miongoni mwa kazi ambazo wengine wasiokuwa wao walishindwa kuzifanya. Na pia alimtiisgia upepo ambao safari yake ya asubuhi ni mwendo wa mwezi mmoja, na safari yake ya jioni ni mwendo wa mwezi mmoja. "Hakika hii" ambayo Mwenyezi Mungu ametupatia, na akatuboresha kwayo "ni fadhila iliyo dhahiri" na ya waziwazi. Kwa hivyo akakiri kukiri kamili zaidi neema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.