انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النمل
السورة ٢٧

النمل

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١١

إِلَّا مَن ظَلَمَ ثُمَّ بَدَّلَ حُسْنًۢا بَعْدَ سُوٓءٍ فَإِنِّى غَفُورٌ رَّحِيمٌ ١١

{11} "Lakini aliyedhulumu, kisha akabadilisha wema baada ya ubaya." Yaani, hiyo ndiyo sababu ya kuwa na hofu na upweke; kwa sababu ya dhuluma aliyofanya na uhalifu aliotenda hapo awali. Na ama mitume, hao wana nini cha kuwafanya wawe na upweke na hofu? Hata hivyo, yeyote anayejidhulumu mwenyewe kwa kumuasi Mwenyezi Mungu kisha akatubu na akarudi kwake, na akabadilisha dhambi zake zikawa matendo mazuri, na uasi wake ukawa utiifu; basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu. Kwa hivyo, mtu yeyote hafai kukata tamaa na rehema yake na msamaha wake; kwani Yeye husamehe dhambi zote, na Yeye ni Mwingi wa rehema kwa waja wake kuliko mama kwa mwanawe.