الشعراء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
قَالُوا۟ وَهُمْ فِيهَا يَخْتَصِمُونَ ٩٦ تَٱللَّهِ إِن كُنَّا لَفِى ضَلَـٰلٍ مُّبِينٍ ٩٧ إِذْ نُسَوِّيكُم بِرَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ ٩٨ وَمَآ أَضَلَّنَآ إِلَّا ٱلْمُجْرِمُونَ ٩٩ فَمَا لَنَا مِن شَـٰفِعِينَ ١٠٠ وَلَا صَدِيقٍ حَمِيمٍ ١٠١ فَلَوْ أَنَّ لَنَا كَرَّةً فَنَكُونَ مِنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ ١٠٢ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةً ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ ١٠٣ وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ ١٠٤
{96-104} "Watasema;" yaani, askari wa Iblisi ambao walipotea wakiwaambia masanamu yao ambayo waliyoyaabudu, "Tallahi! (Kwa jina la Mwenyezi Mungu!) Kwa yakini tulikuwa katika upotovu ulio dhahiri. Tulipowafanya nyinyi ni sawa na Mola Mlezi wa walimwengu wote," katika ibada, upendo, hofu na matumaini, na tunawaomba kama tunavyomuomba Yeye. Kisha hapo ukawawia wazi upotovu wao, na wakakiri uadilifu wa Mwenyezi Mungu katika kuwaadhibu, na kwamba adhabu hiyo ilifaa. Nao hawakuwasawazisha na Mola Mlezi isipokuwa katika ibada, siyo katika uumbaji; kwa ushahidi wa kauli yao, "na Mola Mlezi wa walimwengu wote" kwamba wanakiri kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mola Mlezi wa walimwengu wote, ambao miongoni mwao ni yao masanamu yao na viabudiwa vyao vinginevyo, "Na hawakutupoteza;" tukaacha njia ya uwongofu na unyoofu, na akatuia kupotoka na kuvuka mipaka "isipokuwa wahalifu". Nao ni wale viongozi ambao wanalingania kwenda Motoni. "Basi hatuna waombezi wowote" wakati huo, ambao watatuombea ili watuokoe kutokana na adhabu yake. "Wala rafiki wa dhati" atakayetunufaisha hata kidogo tu, kama ilivyokuwa desturi duniani kufanya hivyo. Kwa hivyo wakakata tamaa juu ya heri yoyote, na wakaangamizwa kwa sababu ya yale waliyoyachuma, na wakatamani kurudi duniani ili watende wema. "Laiti tungelipata kurejea tena" duniani, "tungelikuwa katika Waumini" ili tusalimike kutokana na adhabu na tupate thawabu. Hayawi! Hayawi, tayari imezuiliwa kati yao na kile wanachotamani, na njia zao zote tayari zimeshafungwa. "Hakika katika haya" ambayo tumewatajia na kuwaelezea, "kuna ishara" kwenu "lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini" hata pamoja na kuteremka kwa ishara hizi.