الشعراء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَلَا تُخْزِنِى يَوْمَ يُبْعَثُونَ ٨٧ يَوْمَ لَا يَنفَعُ مَالٌ وَلَا بَنُونَ ٨٨ إِلَّا مَنْ أَتَى ٱللَّهَ بِقَلْبٍ سَلِيمٍ ٨٩
{87-89} "Wala usinihizi Siku watakapofufuliwa" kwa kunikemea juu ya baadhi ya dhambi, na kuniadhibu juu yake na kunifedhehesha. Bali nifurahishe siku hiyo ambayo mali haitafaa kitu wala wana. "Isipokuwa mwenye kumjia Mwenyezi Mungu na moyo safi." Huyu ndiye atakayenufaika kwako, na huyu ndiye atakayeepuka adhabu na kustahili thawabu nyingi. Na maana ya moyo safi ni moyo uliosalimika kutokana na ushirikina, shaka, kupenda uovu, kuendelea kufanya uzushi katika dini na madhambi. Na inalazimu moyo unaposalimika kutokana na hayo yaliyotajwa usifike na kinyume, chake kama vile kumkusudia Mwenyezi Mungu peke yake, elimu, yakini, na kupenda heri, na kuupamba moyo wake na heri hiyo, na kwamba mapenzi yake na upendo yawe ni yenye kufuata upendo wa Mwenyezi Mungu, na matamanio yake yawe yanfuatana na kile kilichotoka kwa Mwenyezi Mungu.