الشعراء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
رَبِّ هَبْ لِى حُكْمًا وَأَلْحِقْنِى بِٱلصَّـٰلِحِينَ ٨٣ وَٱجْعَل لِّى لِسَانَ صِدْقٍ فِى ٱلْـَٔاخِرِينَ ٨٤
{83-84} Kisha yeye amani imshukie akamwita Mola wake Mlezi, akasema, "Mola wangu Mlezi! Nitunukie hukumu;" yaani, elimu nyingi nitakayojua kwayo hukumu, halali, haramu, na nihukumu kwayo kati ya viumbe. "Na uniunganishe na walio wema," miongoni mwa ndugu manabii na mitume. "Na unijalie nitajwe kwa wema na watu watakaokuja baadaye," hadi mwisho wa zama. Mwenyezi Mungu akaitikia maombi yake, na akamtunuku elimu na hukumu ambapo kwa hivyo alikuwa katika Mitume bora zaidi, na akamuunganisha na ndugu zake Mitume, na akamfanya kupendwa, kukubaliwa, kupewa taadhima, kusifiwa katika dini zote katika nyakati zote. Yeye Mtukufu alisema, "Na tukamwachia (sifa njema) kwa watu waliokuja baadaye. Iwe salama kwa Ibrahim! Hivi ndivyo tunavyowalipa wanaofanya mema. Hakika yeye ni katika waja wetu waumini."