انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الشعراء
السورة ٢٦

الشعراء

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآيات ٦٣–٦٨

فَأَوْحَيْنَآ إِلَىٰ مُوسَىٰٓ أَنِ ٱضْرِب بِّعَصَاكَ ٱلْبَحْرَ ۖ فَٱنفَلَقَ فَكَانَ كُلُّ فِرْقٍ كَٱلطَّوْدِ ٱلْعَظِيمِ ٦٣ وَأَزْلَفْنَا ثَمَّ ٱلْـَٔاخَرِينَ ٦٤ وَأَنجَيْنَا مُوسَىٰ وَمَن مَّعَهُۥٓ أَجْمَعِينَ ٦٥ ثُمَّ أَغْرَقْنَا ٱلْـَٔاخَرِينَ ٦٦ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةً ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ ٦٧ وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ ٦٨

{63-68} "Na tulimletea Musa ufunuo tukamwambia: Piga bahari kwa fimbo yako," naye akaipiga. "Basi ikatengana" njia kumi na mbili. "Na kila sehemu ikawa kama mlima mkubwa." Kwa hivyo, Musa na watu wake wakaingia ndani yake. "Na tukawasongesha" mahali "hapo karibu wale wengine." Yaani, Firauni [na] watu wake, na tukawaleta karibu, kisha tukawaingiza katika njia hiyo ambayo Musa na watu wake walipitia. "Tukawaokoa Musa na wale waliokuwa pamoja naye wote." Na wakatoka nje wote bila ya yeyote miongoni mwao kusalia nyuma. "Kisha tukawazamisha hao wengine," na hakuna hata mmoja wao aliyeachwa nyuma ya kuzama. "Hakika bila ya shaka katika hayo ipo Ishara" kubwa juu ya ukweli wa kile ambacho Musa, amani iwe juu yake, alikuja nacho, na ubatili wa kile Firauni na watu wake walikuwa juu yake. "Lakini wengi wao si wenye kuamini," hata pamoja na ishara hii inayolazimu mtu kuamini, kwa sababu ya uharibifu wa nyoyo zenu. "Na kwa hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu, Mwingi wa kurehemu." Kwa nguvu yake, aliwaangamiza makafiri waliokadhibisha, na kwa rehema yake, alimuokoa Musa na wale waliokuwa pamoja naye wote.