الشعراء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَأَوْحَيْنَآ إِلَىٰ مُوسَىٰٓ أَنْ أَسْرِ بِعِبَادِىٓ إِنَّكُم مُّتَّبَعُونَ ٥٢
{52} Kisha Firauni na kaumu yake hawakuacha kuendelea na ukafiri wao. Musa akawa anawajia na ishara zilizo wazi, na kila ilipowajia ishara, na ikawafikia kila kiasi; walimuahidi Musa na kuagana naye kwamba Mwenyezi Mungu akiwaondolea balaa, basi bila shaka watamwamini na bila shaka watawaachilia Wana wa Israili pamoja naye. Basi Mwenyezi Mungu anakuwa ni mwenye kuwaondolea balaa, kisha wao wanaivunja ahadi yao hiyo. Na wakati Musa alipokata tamaa na imani yao, na wakastahiki neno la adhabu, na wakati ukafika wa Wana wa Israili kuokolewa na Mwenyezi Mungu kutoka utumwani kwao na kuwaimarisha katika ardhi, Mwenyezi Mungu akamfunulia Musa, "Nenda na waja wangu wakati wa usiku," mwanzoni mwake, ili wapate kwenda mbali na kwenda kwa mwendo wa polepole bila ya haraka. "Kwa hakika mtafuatwa" na Firauni na majeshi wake. Na likatokea kama alivyojulisha. Kwa maana walipofika asubuhi, tazama, Wana wa Israili wote walikuwa wametoka usiku pamoja na Musa.