انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الشعراء
السورة ٢٦

الشعراء

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآيات ٤٣–٤٥

قَالَ لَهُم مُّوسَىٰٓ أَلْقُوا۟ مَآ أَنتُم مُّلْقُونَ ٤٣ فَأَلْقَوْا۟ حِبَالَهُمْ وَعِصِيَّهُمْ وَقَالُوا۟ بِعِزَّةِ فِرْعَوْنَ إِنَّا لَنَحْنُ ٱلْغَـٰلِبُونَ ٤٤ فَأَلْقَىٰ مُوسَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِىَ تَلْقَفُ مَا يَأْفِكُونَ ٤٥

{43-45} Walipokutana kwa ajili ya miadi, wao, Musa, na watu wa Misri; Musa aliwaaidhi na kuwakumbusha na akasema, "Ole wenu! Msimzulie Mwenyezi Mungu uwongo, asije akawafutilia mbali kwa adhabu. Na mwenye kuzua lazima ashindwe!" Kwa hivyo wakavutana na kugombana, kisha Firauni akawatia moyo nao wakatiana moyo wao kwa wao. "Musa akwaambia: Tupeni mnavyotaka kutupa," miongoni mwa vilivyo katika mawazo yenu. Na wala hakuwazuilia katika wanachofaa kutupa, kwa kuwa alikuwa na hakika kwamba walivyokuja navyo vya kupinga haki ni batili. "Basi wakatupa kamba zao na fimbo zao" na tazama vikawa nyoka wanaokwenda mbio, na wakayafanyia macho ya watu uchawi kwa hayo. "na wakasema: Kwa nguvu za Firauni hakika sisi hapana shaka ni wenye kushinda." Kwa hivyo, wakawa wametafuta msaada wa mja dhaifu kwa njia zote, lakini alikuwa na kiburi na akapata mfano wa ufalme na majeshi, kwa hivyo kiburi hicho kikawadanganya, na ufahamu wao haukupenya ukafikia uhakika wa jambo hilo, au kwamba waliapa kwa nguvu za Firauni, na kilichoapwa kufanywa ni kwamba watashinda. "Basi Musa akatupa fimbo yake, nayo mara ikavimeza walivyovizua," vya vile kamba na fimbo, kwa sababu vilikuwa uzushi na uwongo na udanganyifu, na hayo yote ni batili ambayo haiwezi kusimama mbele ya haki wala kuipinga.