انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الشعراء
السورة ٢٦

الشعراء

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآيات ٢٩–٣٣

قَالَ لَئِنِ ٱتَّخَذْتَ إِلَـٰهًا غَيْرِى لَأَجْعَلَنَّكَ مِنَ ٱلْمَسْجُونِينَ ٢٩ قَالَ أَوَلَوْ جِئْتُكَ بِشَىْءٍ مُّبِينٍ ٣٠ قَالَ فَأْتِ بِهِۦٓ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّـٰدِقِينَ ٣١ فَأَلْقَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِىَ ثُعْبَانٌ مُّبِينٌ ٣٢ وَنَزَعَ يَدَهُۥ فَإِذَا هِىَ بَيْضَآءُ لِلنَّـٰظِرِينَ ٣٣

{29-33} Na hoja hiyo ilipomnyonga Firauni, na uwezo wake na kueleza kwake kukashindwa kupinga kitu, "akasema" huku akimtishia Musa kwa mamlaka yake; "Ukimfuata mungu mwingine asiyekuwa mimi, basi bila ya shaka nitakufunga gerezani." Kwa hivyo, akawa amedai - Mwenyezi Mungu amlaani - kwamba anatamani kumpoteza Musa, na kwamba asimchukue mungu mwingine. Vinginevyo, ilikwisha julikana kwamba yeye na wale walio pamoja naye walikuwa wanajua vyema jambo lao. Kwa hivyo, Musa akamwambia, "Je, ijapokuwa nitakuletea kitu cha kubainisha wazi?" Kitakachoonyesha usahihi wa kile nilichokujia nacho katika mambo yasiyo ya kawaida? "Akasema: Kilete basi, kama wewe ni katika wakweli." "Basi akaitupa fimbo yake, mara ikawa nyoka wa kuonekana dhahiri." Naye alikuwa nyoka wa kiume, anayemuonekania kila mtu kwa njia dhahiri isiyokuwa na hila yoyote wala kufananisha. "Na akautoa mkono wake" kutoka mfukoni mwake, "na mara ukawa mweupe kwa watazamao." Yaani, ulikuwa na nuru kubwa ambayo haina upungufu wowote kwa wale wanaoiangalia.