انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الشعراء
السورة ٢٦

الشعراء

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآيات ١٠–١١

وَإِذْ نَادَىٰ رَبُّكَ مُوسَىٰٓ أَنِ ٱئْتِ ٱلْقَوْمَ ٱلظَّـٰلِمِينَ ١٠ قَوْمَ فِرْعَوْنَ ۚ أَلَا يَتَّقُونَ ١١

Yeye Muumba Mtukufu alirudia kisa cha Musa Qur-ani na kukisisitiza kwa namna ambayo hakukirudia kisa kinginecho, kwa sababu kinajumuisha hekima kubwa na mazingatia. Na kina habari zake na madhalimu na waumini, naye ndiye alipewa Sheria Kuu, na akapewa Taurati, kitabu bora zaidi baada ya Qur-ani. Akasema:

{10-11} Na itaje hali nzuri ya Musa wakati Mwenyezi Mungu alipomuita, akamzungumzisha na akamfanya kuwa Nabii na Mtume. Akasema, "Nenda kwa kaumu madhalimu" ambao walitakabari katika ardhi, na wakajiinua juu ya watu wake mpaka mkubwa wao akadai uungu. "Kaumu wa Firauni. Kwani hawamchi Mwenyezi Mungu?" Yaani, waambie kwa maneno laini na usemi wenye upole. Kwani hawamchi Mwenyezi Mungu ambaye aliwaumba na akawaruzuku, basi mkaachana na huo ukafiri mnaofanya?