انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الفرقان
السورة ٢٥

الفرقان

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٧٢

وَٱلَّذِينَ لَا يَشْهَدُونَ ٱلزُّورَ وَإِذَا مَرُّوا۟ بِٱللَّغْوِ مَرُّوا۟ كِرَامًا ٧٢

{72} "Na wale ambao hawatoi ushahidi wa uongo" sawa iwe kauli au vitendo vilivyoharamishwa. Kwa hivyo wakawa wanajiepusha na vikao vyenye maneno yaliyoharamishwa au vitendo vilivyoharamishwa, kama vile kuingia katika ishara za Mwenyezi Mungu, kujadili kwa batili, kusengenya, kufitini, kutukana, kuzulia watu machafu, kufanya stihizai, kuimba kwa haramu, kunywa mvinyo, kukatia hariri, na picha, na mfano wa hayo. Na ikiwa hawashuhudii uongo, basi inawafailia zaidi kutousema na kutoufanya. Na ushahidi wa uongo unajumuishwa katika kusema uongo, na hilo linaingia katika aya hii kwa namna ya kufailia zaidi. "Na pindi wapitapo penye upuuzi" ambao ni maneno ambayo hayana heri yoyote wala faida ya kidini wala ya kidunia, kama vile maneno ya wapumbavu na mfano wao. "Hupita kwa heshima yao;" yaani, wanajitakasa nafsi zao na kuzitukuza dhidi ya kujiingiza ndani yake, na kuona kuingia ndani yake hata ikiwa hakuna dhambi ndani yake. Kwa maana ni upumbavu na upungufu katika ubinadamu na utu, kwa hivyo wakajiinua kutokana na hayo. Na katika kauli yake; "Na pindi wapitapo penye upuuzi," kuna ishara kwamba hawakusudii kuhudhuria penye upuuzi wala hata kuusikia, lakini wakikutana nao kwa bahati mbaya tu bila ya kukusudia, basi wanajiheshimu wakajitenga mbali nao.