الفرقان
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَهُوَ ٱلَّذِى جَعَلَ ٱلَّيْلَ وَٱلنَّهَارَ خِلْفَةً لِّمَنْ أَرَادَ أَن يَذَّكَّرَ أَوْ أَرَادَ شُكُورًا ٦٢
{62} "Naye ndiye aliyefanya usiku na mchana kufuatana" milele na wala havikutani wala haviondoki vyote. "Kwa nafuu ya yule anayetaka kukumbuka, au anayetaka kushukuru." Na avitumie kama ushahidi juu ya matashi mengi ya kimungu. Basi ana zamu katika usiku au mchana. Na mwenye kupitwa na zamu yake katika moja yake, anaweza kuipata katika ile nyingine. Na tena kwa upande mwingine, mioyo hubadilika na kugeuka katika masaa ya usiku na mchana, kwa hivyo inakuwa na nguvu, uvivu, kukumbuka, kughafilika, kujikunja, kupanuka, kukubali mambo na kuyakataa. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu akafanya usiku na mchana kuwajia waja kwa kufuatana na kurudia; ili kwa viwili hivyo awafanye kukumbuka, kuwa na nguvu, na kumshukuru Mwenyezi Mungu wakati mwingine. Na kwa sababu nyakati za ibada hurudia kwa sababu ya kurudiarudia kwa usiku na mchana. Na kila nyakati zinaporudia, hilo linamfanya mja kuwa na hima isiyokuwa hima ile iliyokuwa imezembea katika wakati uliopita, kwa hivyo wakazidi kukumbuka na kushukuru. Na kazi ya mambo ya utii ni kama kuinywesha imani na kuizidisha. Na kama haingekuwa hivyo, basi mmea wa imani ungefifia na kukauka. Basi ni za Mwenyezi Mungu sifa kamili juu ya hilo.