الفرقان
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَنفَعُهُمْ وَلَا يَضُرُّهُمْ ۗ وَكَانَ ٱلْكَافِرُ عَلَىٰ رَبِّهِۦ ظَهِيرًا ٥٥
{55} Yaani, wanaabudu masanamu na wafu ambao hawadhuru wala hawafaidi, na wanawafanya kuwa wenza wa Mmiliki wa kunufaisha na kudhuru, kupeana na kuzuia, pamoja na kwamba la wajibu juu yao ni kwamba wafuate maelekezo ya Mola wao Mlezi, wakiitetea Dini yake. Lakini wao walifanya kinyume cha hilo. "Na kafiri daima ni msaidizi wa kumpinga Mola wake Mlezi." Kwa maana batili ambayo ni vyote viabudiwavyo badala ya Mwenyezi Mungu na wale wawafanyao kuwa wenza wake ni maadui wa Mwenyezi Mungu. Naye kafiri alivisaidia na kuviunga mkono dhidi ya Mola wake Mlezi, na akawa adui wa Mola wake Mlezi, akajitokeza mbele yake kupambana dhidi yake kwa uadui na vita. Huyu ndiye ambaye Mwenyezi Mungu alimuumba, akamruzuku na akamneemesha kwa neema dhahiri na zilizofichika, na tena hawezi toka katika ufalme wake, mamlaka yake na mshiko wake, na Mwenyezi Mungu hakumkatia hisani yake na wema wake, lakini yeye kwa ujinga wake anaendelea na uadui huu na mapambano haya.