الفرقان
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
ٱلَّذِينَ يُحْشَرُونَ عَلَىٰ وُجُوهِهِمْ إِلَىٰ جَهَنَّمَ أُو۟لَـٰٓئِكَ شَرٌّ مَّكَانًا وَأَضَلُّ سَبِيلًا ٣٤
{34} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu hali ya washirikina ambao walimkadhibisha Mtume wake na hatima yao mbaya, na kwamba, "watakusanywa kwa nyuso zao," katika mwonekano mbaya zaidi na katika mandhari ya kutisha zaidi. Malaika wa adhabu watawavuta na kuwaburura, "hadi katika Jahannamu" ambayo imejumuisha kila adhabu na mateso. "Hao" walio katika hali hii ndio "watakuwa na mahali pabaya mno" kuliko wale waliomwamini Mwenyezi Mungu na wakawasadiki Mitume wake. "Nao ndio wenye kuipotea zaidi njia." Na hii ni katika mbinu ya kutumia njia ya kuboresha kati ya mambo ambayo ubora huo uko upande mmoja tu. Kwa maana, waumini wana mahali na maskani pazuri zaidi, na tena duniani waliongoka hadi kwenye njia iliyonyooka, na wakaongoKa katika Akhera kufikia bustani za neema.