الفرقان
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَا لِكُلِّ نَبِىٍّ عَدُوًّا مِّنَ ٱلْمُجْرِمِينَ ۗ وَكَفَىٰ بِرَبِّكَ هَادِيًا وَنَصِيرًا ٣١
{31} Naye Mwenyezi Mungu akasema huku akimliwaza Mtume wake na akimjulisha kwamba: Hakika viumbe hawa wana watangulizi waliofanya kama walivyofanya hawa. Na akasema, "Na vivyo hivyo tumemfanyia kila Nabii adui miongoni mwa wahalifu," miongoni mwa wale ambao hawaifailii heri wala hawatakasiki kwayo. Wale wanaowapinga, na kuwakataa, na wanajadiliana nao kwa batili. Na baadhi ya faida za hili ni haki kuwa juu ya batili, na kubainika kwa haki na kuwa wazi kwa uwazi mkubwa, kwa sababu batili kuipinga haki kunaiongezea uwazi, na kuwa kwake ushahidi kamilifu, na ili tuone kile ambacho Mwenyezi Mungu anawafanyia wana haki kama vile kuwatukuza, na kile anachowafanyia wana batili kama vile kuwaadhibu. Kwa hivyo usiwahuzunikie, wala nafsi yako isijihiliki kwa kuwahuzunikia. "Na Mola wako Mlezi anatosha kuwa Mwenye kuongoa;" mwenye kukuongoa ukapata kile unachohitaji na masilahi ya dini yako na dunia yako. "Na Mwenye kunusuru," atakayekunusuru dhidi ya maadui zako, na kukuzuilia na kila la kuchukiza katika mambo ya dini na dunia. Kwa hivyo jitosheleze naye na umtegemee.