الفرقان
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
لَّقَدْ أَضَلَّنِى عَنِ ٱلذِّكْرِ بَعْدَ إِذْ جَآءَنِى ۗ وَكَانَ ٱلشَّيْطَـٰنُ لِلْإِنسَـٰنِ خَذُولًا ٢٩
{29} "Hakika alinipoteza, nikaacha ukumbusho, baada ya kwisha nijia;" ambapo alimpambia yale anayoyafanya ya upotofu kwa kumhadaa na kumshawishi. "Na kweli Shetani ni haini mkubwa kwa mwanadamu." Yeye humpambia batili na kumfanya kuona kwamba haki ni mbaya, na anamuahidi matarajio, kisha akamwacha na kumkana. Kama alivyowaambia wafuasi wake wote wakati jambo lilipoamuliwa, na Mwenyezi Mungu akamaliza kuwafanyia hesabu viumbe. "Na Shetani atasema itakapokatwa hukumu: Hakika Mwenyezi Mungu aliwaahidi ahadi ya haki. Nami nakawaahidi; lakini sikuwatimizia. Na sikuwa na mamlaka yoyote juu yenu, isipokuwa tu kwamba niliwaita, nanyi mkaniitikia. Basi msinilaumu mimi, bali jilaumuni wenyewe. Mimi siwezi kuwa mtetezi wenu, wala nyinyi hamuwezi kuwa watetezi wangu. Hakika mimi nilikataa tangu zamani kunishirikisha kwenu na Mwenyezi Mungu..." hadi mwisho wa Aya. Basi mja na ajiangalilie kama bado inawezekana, na akimbilie kufanya yale yanayowezekana kabla hayajafikia kutowezekana, na amfanye kipenzi yule ambaye katika kumfanya kipenzi kuna furaha yake, na amfanye adui yule ambaye kunamnufaisha kumfanyia uadui na kunamdhuru kufanya urafiki naye. Na Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kuwezesha.