النور
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَأَقِيمُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُوا۟ ٱلزَّكَوٰةَ وَأَطِيعُوا۟ ٱلرَّسُولَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ٥٦
{56}Mwenyezi Mungu anaamrisha kusimamisha Swala pamoja na nguzo zake, masharti yake, na adabu zake, kwa nje na ndani, na kwa kutoa zaka kutokana na mali ambayo Mwenyezi Mungu amewateua waja kuwa warithi na akawapa; kwa kuwapa masikini na wengine ambao Mwenyezi Mungu amewataja kwa mtoaji wa zaka. Haya ni matendo makuu na adhimu ya utiifu, ambayo ni yenye kukusanya haki zake na haki za viumbe vyake; uaminifu kwa anayeabudiwa, na wema kwa waja. Kisha akawapa amri ya jumla, na akasema: ''Na mtiini Mtume;'' kwa kutii amri zake na kuepuka makatazo yake, ''Na mwenye kumtii Mtume basi amemtii Mwenyezi Mungu,'' ''pengine nyinyi,'' mnapofanya hivyo, ''ili mpate kurehemewa.'' Basi mwenye kutaka rehema; hii ndiyo njia yake, na anayeitaraji bila ya kuswali, kutoa zaka, na kumtii Mtume; Yeye ni mwotaji wa uongo, na nafsi yake imempa matamanio ya uongo.