النور
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
قُلْ أَطِيعُوا۟ ٱللَّهَ وَأَطِيعُوا۟ ٱلرَّسُولَ ۖ فَإِن تَوَلَّوْا۟ فَإِنَّمَا عَلَيْهِ مَا حُمِّلَ وَعَلَيْكُم مَّا حُمِّلْتُمْ ۖ وَإِن تُطِيعُوهُ تَهْتَدُوا۟ ۚ وَمَا عَلَى ٱلرَّسُولِ إِلَّا ٱلْبَلَـٰغُ ٱلْمُبِينُ ٥٤
{54} Hii ndiyo hali yao katika jambo hilo hilo, na ama Mtume Rehema za Mwenyezi Mungu na Amani zimshukie yeye; kazi yake ni kuwaamrisha na kuwakataza. Na ndiyo maana akasema: "Sema, Mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume" wakamtii; Ilikuwa ni bahati yenu na furaha yenu. ''Na mkigeuka, basi yaliyo juu yake ni yale aliyobebeshwa'' katika Ujumbe, naye ameutimiza. ''Na yaliyo juu yenu ni yale mliyobebshwa nyinyi,'' kutokamana na utiifu, na hakika hali yenu imedhihirika, na ukadhihirika upotofu wenu na mkastahili nyinyi adhabu. ''Na mkimtii yeye mtaongoka,'' kwenye njia iliyonyooka kwa maneno na matendo; hakuna njia ya nyinyi kuongoka isipokuwa kwa kumtii yeye, vinginevyo haiwezekani, bali hiyo haiwezekani. ''Na hapana juu ya Mtume ila ni kufikisha Ujumbe wazi wazi;'' Yaani, kuwafikishia habari zilizo wazi zisizoacha shaka wala wahaka kwa yeyote. Na hakika alifanya Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema za Mwenyezi Mungu na amani zimshukie yeye; alifikisha ujumbe ulio wazi, na hakika anayewahisabu na kuwalipa malipo ni Mwenyezi Mungu Mtukufu. Mjumbe hakuwa na uhusiano wowote na jambo hilo, alisimama na kutekeleza kazi yake.