النور
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَإِن يَكُن لَّهُمُ ٱلْحَقُّ يَأْتُوٓا۟ إِلَيْهِ مُذْعِنِينَ ٤٩
{49}''Na ikiwa haki ni yao, wanamjia,'' kwa hukumu ya kisheria ''kwa kumtii.'' Hii si kwa sababu ni hukumu halali, bali ni kwa ajili ya kukubaliana na matamanio yao. Hawasifiwi katika hali hii, hata wakimjia kwa kunyenyekea. Kwa sababu mja wa kweli ni yule anayefuata haki katika yale ayapendayo na anayoyachukia, na yale yanayomfurahisha na yanayomhuzunisha. Ama mwenye kufuata sheria inapoafikiana na matamanio yake na akaikataa inapopingana nayo, na akaweka matamanio yake mbele ya sheria; yeye si mtumwa katika hali halisi.