انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النور
السورة ٢٤

النور

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٢٢

وَلَا يَأْتَلِ أُو۟لُوا۟ ٱلْفَضْلِ مِنكُمْ وَٱلسَّعَةِ أَن يُؤْتُوٓا۟ أُو۟لِى ٱلْقُرْبَىٰ وَٱلْمَسَـٰكِينَ وَٱلْمُهَـٰجِرِينَ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ ۖ وَلْيَعْفُوا۟ وَلْيَصْفَحُوٓا۟ ۗ أَلَا تُحِبُّونَ أَن يَغْفِرَ ٱللَّهُ لَكُمْ ۗ وَٱللَّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ٢٢

{22} "Na wale katika nyinyi wenye fadhila na wasaa wasiape kutowapa jamaa zao, na masikini na waliohama kwa Njia ya Mwenyezi Mungu. Na wasamehe, na waachilie mbali." Katika jumla ya waliojihusisha na uzushi ni Mistah bin Uthathah ambaye alikuwa ni ndugu wa Abu Bakr Al-Siddiq, Mungu amuwiye radhi. Alikuwa Mistah ni masikini aliyehama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Na akaapa Abu Bakr kutotumia na kutoa juu yake kwa sababu ya yale aliyoyasema. Basi ikateremshwa Aya hii "ikimkataza" kutokana na kiapo hiki kilichojumuisha kukata riziki yake, na kumhimiza amsamehe na aachilie mbali jambo hilo, na kumuahidi msamaha wa Mwenyezi Mungu ikiwa atamsamehe. Basi akasema, "Je, nyinyi hampendi Mwenyezi Mungu awasamehe? Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu." Mkiwafanyia waja wake msamaha; naye Mwenyezi Mungu atawafanyia hivyo. Na Abu Bakr akasema aliposikia aya hii, 'Ndiyo, Wallahi (Naapa kwa jina Mwenyezi Mungu); ningependa Mwenyezi Mungu anisamehe. Na kurudisha kutoa na kutumia kwa Mistah. Na katika aya hii ni ushahidi juu kuwapa riziki jamaa wa karibu wa mtu, na kwamba matumizi na ihsani haziachwi wala kupuuzwa na uasi wa mtu. Na kuhimiza kusamehe hata kama kile kilichotokea kutoka kwake kilitokea kwa watu wa uhalifu.