انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · المؤمنون
السورة ٢٣

المؤمنون

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٢٤

فَقَالَ ٱلْمَلَؤُا۟ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ مِن قَوْمِهِۦ مَا هَـٰذَآ إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ يُرِيدُ أَن يَتَفَضَّلَ عَلَيْكُمْ وَلَوْ شَآءَ ٱللَّهُ لَأَنزَلَ مَلَـٰٓئِكَةً مَّا سَمِعْنَا بِهَـٰذَا فِىٓ ءَابَآئِنَا ٱلْأَوَّلِينَ ٢٤

{24} Basi akaendelea hivyo kuwalingania kwa siri, waziwazi, usiku na mchana kwa miaka elfu moja, isipokuwa miaka hamsini. Na wao wakawa hawazidishi isipokuwa kiburi na kujiweka mbali. "Wakasema wale wakuu" kutoka katika kaumu yake, waheshimiwa na mabwana wanaofuatwa, kwa njia ya kumpinga Nabii wao Nuhu na kutahadharisha dhidi ya kumfuata, "Huyu si chochote isipokuwa ni mtu tu kama nyinyi. Anataka kujipa ubora juu yenu;" ili ufuatwe. Vinginevyo, ni nini kinachomfanya kuwa bora zaidi yenu, naye ni wa aina yenu? Na upinzani huu haujaacha kuwapo katika wale wanaowakadhibisha Mitume. Na Mwenyezi Mungu alijibu hilo kwa jibu la kutosha, juu ya ndimi za Mitume wake. Kama katika kauli yake, "Wakasema;" yaani, wakiwaambia mitume wao, "Nyinyi si chochote isipokuwa watu kama sisi. Mnataka kutuzuilia na yale waliyokuwa wakiabudu baba zetu. Basi tuleteeni hoja iliyo wazi. Mitume wao wakawaambia: Sisi kweli si chochote isipokuwa ni watu kama nyinyi. Lakini Mwenyezi Mungu humfanyia hisani amtakaye katika waja wake." Basi wakawajulisha kwamba hii ni fadhila ya Mwenyezi Mungu na neema yake. Nanyi hamuwezi kumkataza Mwenyezi Mungu, na kumzuia kutufikishia fadhila yake. Pia wakasema, "Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angetaka, basi kwa yakini angeliteremsha Malaika." Na hili pia ni pingamizi batili la kutumia majaliwa ya Mwenyezi Mungu kuwa ndiyo hoja. Kwani, hata kama angelitaka, angeliteremsha Malaika, yeye ni Mwenye hekima, Mwingi wa kurehemu. Hekima yake na rehema yake vinataka kwamba Mtume awe wa jamii ya binadamu, kwa sababu wao hawana uwezo wa kuwaongelesha Malaika, wala hawezi kuwa isipokuwa na umbo la mtu, kisha tena watachanganyikiwa tu kama ilivyokuwa. Na kauli yao, "Hatukuyasikia haya" ya kumtuma Mtume "kwa baba zetu wa mwanzoni." Lakini kuna hoja gani kwamba hawakusikia kutumwa kwa Mtume kwa baba zao wa mwanzoni? Kwa sababu wao hawakuzunguka kwa elimu hayo yaliyopita kitambo. Kwa hivyo hawafanyi kutumia ujinga wao kuwa ndiyo hoja yao! Na hata ikiwa itachukuliwa kwamba hakumtuma mtume kutoka kwao, basi ima wao walikuwa katika uwongofu, kwa hivyo hakuna haja ya kumtuma mtume wakati huo, au walikuwa vinginevyo, kwa hivyo hawa na wamsifu na kumshukuru Mola wao Mlezi kwa sababu aliwateua kwa neema ambayo haikuwahi kuwafikia baba zao wala hawakuwahi kuihisi, na tena hawafai kufanya kutoneemeshwa wengineo kuwa ndiyo sababu ya kukufuru kwao wema waliofanyiwa wao.