انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الحج
السورة ٢٢

الحج

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٧٠

أَلَمْ تَعْلَمْ أَنَّ ٱللَّهَ يَعْلَمُ مَا فِى ٱلسَّمَآءِ وَٱلْأَرْضِ ۗ إِنَّ ذَٰلِكَ فِى كِتَـٰبٍ ۚ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى ٱللَّهِ يَسِيرٌ ٧٠

{70} Na katika sehemu ya ukamilifu wa hukumu yake ni kwamba awe mtawala mwenye elimu; ndiyo maana akataja upana wa elimu yake na upana wa kitabu chake. Na akasema, "Je, hukujua kwamba Mwenyezi Mungu anayajua yaliyomo mbinguni na ardhini?" Hakuna kinachofichika kwake katika mambo yaliyo ya dhahiri na mambo ya siri ya mambo; ya siri na dhahiri, ya mwanzo na ya mwisho. Hiyo ni elimu inayozunguka vilivyomo mbinguni na ardhini, Mwenyezi Mungu ameithibitisha katika Kitabu, ambacho ni: Ubao Uliohifadhiwa, pale Mwenyezi Mungu alipoumba kalamu, akaiambia; 'Andika!' Ikasema: 'Niandike nini?' Akasema: 'Andika yatakayotokea mpaka Siku ya Kiyama.' "Hakika haya kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi." Mwenyezi Mungu hufanya yawe rahisi kwake kuwa na ujuzi wa mambo yote, na kuandika hilo katika kitabu kinacholingana na ukweli.