انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الحج
السورة ٢٢

الحج

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٢٥

إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ وَٱلْمَسْجِدِ ٱلْحَرَامِ ٱلَّذِى جَعَلْنَـٰهُ لِلنَّاسِ سَوَآءً ٱلْعَـٰكِفُ فِيهِ وَٱلْبَادِ ۚ وَمَن يُرِدْ فِيهِ بِإِلْحَادٍۭ بِظُلْمٍ نُّذِقْهُ مِنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ ٢٥

{25} Mwenyezi Mungu Mtukufu anaeleza ubaya wa wanayoyafanya washirikina waliomkufuru Mola wao Mlezi, na kwamba wamechanganya kumkufuru Mwenyezi Mungu na Mitume wake, na kuzuilia Njia ya Mwenyezi Mungu, na kuwazuia watu wasiamini, na pia kugeuka. Wakajitenga na Msikiti Mtakatifu ambao si wao wala baba zao, bali walimwacha mbora wa viumbe, Muhammad na maswahaba zake. Hakika ni kuwa Msikiti Mtukufu ni miongoni mwa utakatifu wake, heshima na ukuu wake, na kwamba "kila atakayetaka kufanya upotofu humo kwa dhuluma, basi tutamwonjesha adhabu chungu." Tamaa tu ya dhuluma na ukafiri katika pahali patakatifu inalazimu adhabu, hata kama kuna kitu kisichokuwa hicho, mja haadhibiwi isipokuwa kwa kufanya dhuluma. Basi vipi kuhusu yule aliyefanya dhuluma kubwa zaidi, mfano ukafiri na ushirikina, na kumzuilia njia yake, na kumzuia yeyote anayemtaka kumzuru? Wanafikiri Mungu atawafanya nini? Katika aya hii tukufu, kuna wajibu wa kupaheshimu patakatifu, kuheshimu kwa uthabiti, na kuonya dhidi ya kukusudia na kufanya dhambi ndani yake.