الأنبياء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
لَاهِيَةً قُلُوبُهُمْ ۗ وَأَسَرُّوا۟ ٱلنَّجْوَى ٱلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ هَلْ هَـٰذَآ إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ ۖ أَفَتَأْتُونَ ٱلسِّحْرَ وَأَنتُمْ تُبْصِرُونَ ٣
{3} "Zimeghafilika nyoyo zao" katika kutafuta mambo yao ya kidunia, na miili yao ni yenye kucheza tu. Wameshughulika tu na matamanio na kufanya mambo batili na maneno mabaya, pamoja na kwamba wanapaswa kutokuwa katika sifa hizi. Mioyo yao inakubali amri ya Mwenyezi Mungu na makatazo yake, na kuyasikiliza kusikiliza kwa kufahamu kilichokusudiwa kwayo, na viungo vyao vifanye bidii katika kumwabudu Mola wao Mlezi, ambayo waliumbwa kwa ajili yake, na watie akilini siku ya Qiyama, hesabu na malipo. Na kwa hayo ndiyo mambo yao yanatimia, na hali zao zinanyooka, na matendo yao yanatakasika. Na kuna maana mbili katika kauli yake, "Imewakaribia watu hesabu yao." Moja yake ni kwamba umma huu ndio umma wa mwisho, na Mtume wake ndiye mtume wa mwisho, na Saa ya Qiyama itawasimamia umma wake. Kwa hivyo hesabu imewakaribia wao sana kwa kulinganisha na umma za kabla yao. Kama ilivyo katika kauli yake - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, - "Nimetumwa mimi ilhali Saa ya Qiyama ni kama hivi viwili." Na akaunganisha vidole vyake viwili: cha shahada na kinachokifuata. Na kauli ya pili ni kwamba kile kinachokusudiwa katika kukaribia kwa hesabu ni kifo, na kwamba mwenye kufa, anakuwa ameshasimamiwa na Qiyama yake, na akaingia katika Nyumba ya malipo juu ya matendo. Na kwamba huku ni kumstaajabu kila aliyeghafilika, anayepeana mgongo, asiyejua ni lini yatamjia kwa ghafla mauti, asubuhi au jioni. Na hii ndiyo hali ya watu wote, isipokuwa yule ambaye amepatwa na kujaliwa kwa kiungu, kwa hivyo akajiandaa kwa ajili ya mauti na yaliyoko baada yake. Kisha akataja yale wanayonong'nezana makafiri madhalimu kwa njia ya ukaidi na kuikabili haki kwa batili, na kwamba walinong'onezana na wakakubaliana wao kwa wao kwamba waseme juu ya Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, - 'Hakika, yeye ni mtu mfano wenu. Basi ni nini kilichomfanya kuwa bora juu yenu na kikamfanya kuwa mahsusi miongoni mwenu?' Basi lau kama mmoja wenu angedai mfano wa madai yake, ingekua kauli yake ni ya aina sawa na kauli yake hiyo, lakini yeye anataka tu kujiboresha juu yenu na awe kiongozi wenu. Kwa hivyo msimtii wala msimsadiki, na kwamba yeye hakika ni mchawi, na alichokuja nacho katika Qur-ani ni uchawi. Basi jiepusheni mbali naye, na waepusheni mbali watu naye. Na semeni, "Je, mnauendea uchawi ilhali nyinyi mnaona?" Waliyasema haya ilhali wanajua kwamba kwa kweli yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa sababu ya yale ishara zenye kung'aa wanazozishuhudia, ambazo wasiokuwa wao hawakuwahi kuzishuhudia, lakini upotovu, dhuluma na ukaidi ndiyo yaliwafanya kuwa hivyo.