انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · طه
السورة ٢٠

طه

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٤

تَنزِيلًا مِّمَّنْ خَلَقَ ٱلْأَرْضَ وَٱلسَّمَـٰوَٰتِ ٱلْعُلَى ٤

{4} Kisha akataja utukufu wa Qur-ani hii kuu, na kwamba ni uteremsho wa Muumba wa ardhi na mbingu, Mwendeshaji wa viumbe vyote. Yaani, ukubalini uteremsho wake kwa utiifu mkubwa zaidi, upendo na kujisalimisha, na upeni taadhima kubwa mno. Na mara nyingi inaunganishwa baina ya uumbaji na amri, kama vile katika Aya hii na kama vile katika kauli yake "fahamuni! Kuumba na amri ni zake," na katika kauli yake, "Mwenyezi Mungu ni yule ambaye ameziumba mbingu saba, na ardhi kwa mfano wa hizo. Amri zake zinashuka baina yake." Na hayo ni kwamba Yeye ndiye Muumba, Mwenye kuamrisha, Mwenye kukataza. Na kama vile hakuna muumba yeyote isipokuwa Yeye tu, basi viumbe hawalazimishwi wala kuamrishwa wala kukatazwa isipokuwa na Muumba wao. Na pia, kuna uendeshaji wa kimajaliwa katika kuumba kwake viumbe, nayo amri yake ndani yake kuna uendeshaji wa kisheria wa kidini. Na kama vile kuumba hakutoki nje ya hekima, na hakuumba vitu bure tu, vile vile haamrishi wala hakatazi isipokuwa kwa uadilifu, hekima, na ihsani.