انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · طه
السورة ٢٠

طه

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآيات ١٠٢–١٠٤

يَوْمَ يُنفَخُ فِى ٱلصُّورِ ۚ وَنَحْشُرُ ٱلْمُجْرِمِينَ يَوْمَئِذٍ زُرْقًا ١٠٢ يَتَخَـٰفَتُونَ بَيْنَهُمْ إِن لَّبِثْتُمْ إِلَّا عَشْرًا ١٠٣ نَّحْنُ أَعْلَمُ بِمَا يَقُولُونَ إِذْ يَقُولُ أَمْثَلُهُمْ طَرِيقَةً إِن لَّبِثْتُمْ إِلَّا يَوْمًا ١٠٤

Kisha akaendelea na kutaja hali za Siku ya Qiyama na mambo yake ya kuhofisha, akasema:

Yaani, itakapopulizwa katika baragumu, kisha watu wakatoka makaburini mwao, kila mmoja kulingana na hali yake. Wachamungu watakusanywa kwa Mwingi wa rehema kama wageni wake. Nao wahalifu watakusanywa huku rangi zao ni za buluu kutokana na hofu, wasiwasi na kiu. Watanong'onozana wao kwa wao kuhusiana na namna ulivyokuwa mfupi muda wa dunia na kufika haraka kwa Akhera. Basi baadhi yao watasema: Hamkukaa isipokuwa siku kumi tu. Na baadhi yao watasema yasiyokuwa hayo. Na Mwenyezi Mungu anajua kunong'onozana kwao na anasikia wanayoyasema, "atakaposema mbora wao katika mwendo." Yaani, yule ambaye ni wa wastani wao na aliye karibu zaidi wao katika kukadiria muda waliokaa. "Nyinyi hamkukaa ila siku moja tu." Na makusudio ya haya ni kuonyesha majuto makubwa, jinsi walivyopoteza muda mfupi na kuumaliza huku wamejisahaulisha, kufanya upuuzi, na kuyapa mgongo yale yenye kuwanufaisha, na kuyaendea yale yenye kuwadhuru. Na hapa tayari yamekwisha fika malipo, na tishio la adhabu likatimia, kwa hivyo hakijabakia isipokuwa majuto na kuomba maangamio na kupotelea mbali. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Atasema: Mlikaa muda gani katika ardhi kwa hesabu ya miaka? Watasema: Tulikaa siku moja au sehemu ya siku. Basi waulize wanaoweka hesabu. Atasema: Nyinyi hamkukaa huko duniani isipokuwa kidogo tu, laiti ingelikuwa mnajua."