البقرة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
قُلْ إِن كَانَتْ لَكُمُ ٱلدَّارُ ٱلْـَٔاخِرَةُ عِندَ ٱللَّهِ خَالِصَةً مِّن دُونِ ٱلنَّاسِ فَتَمَنَّوُا۟ ٱلْمَوْتَ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ ٩٤
(94) Yani "Sema" uwaambie katika hali ya kusahihisha madai yao "Ikiwa nyumba ya Akhera ni yenu tu " yani Pepo " bila ya watu wengine" kama mlivyodai kuwa hataingia Peponi ila aliyekuwa Myahudi au Mkristo; na kwamba Moto hautawagusa ila kwa siku chache tu. Basi ikiwa nyinyi ni wakweli katika madai haya, "basi tamanini mauti." Hii ni aina ya mubahala (kulaaniana) baina yao na Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani ziwe juu yake. – Na hakuna baada ya huku kuwalazimisha na kuwafanyia ugumu baada ya ukaidi kutoka kwao ila moja ya mambo mawili: Ima wamuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na ima wafanye mubahala (kulaaniana) kwa yale waliyo juu yake kwa kitu chepesi kwao, ambacho ni kutamani mauti ambayo yatawafikisha kwenye nyumba ambayo ni mahsusi kwao tu. Lakini wakakataa kufanya hivyo, kwa hivyo, kila mtu akajua kwamba wao wanafanya ukaidi mkubwa mno, na kumfanyia uadui Mwenyezi Mungu na Mtume wake, licha ya kujua kwao hilo. Na kwa sababu ya hilo, Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: