انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · البقرة
السورة ٢

البقرة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٨١

بَلَىٰ مَن كَسَبَ سَيِّئَةً وَأَحَـٰطَتْ بِهِۦ خَطِيٓـَٔتُهُۥ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ أَصْحَـٰبُ ٱلنَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَـٰلِدُونَ ٨١

Kisha (Mwenyezi Mungu) Mtukufu akataja hukumu ya jumla kwa kila mtu, wanaingia humo Wana wa Israili na wasiokuwa wao. Nayo ni hukumu ambayo hakuna hukumu ngingine isiyokuwa hiyo, na sio uongo wanaoutamani na madai yao kuhusu walioangamia, na waliofaulu. Hivyo basi akasema "Ndiyo" yani hili jambo sio kama mlivyotaja. Kwani ni kauli tu isiyokuwa na uhakika wowote. Lakini:

(81) "anaye chuma ubaya" Nalo hili neno ni nakira (yani halimaanishi kosa maalum) katika muktadha wa sharti, kwa hivyo linajumuisha shirki na kilicho chini yake, na hapa limekusudiwa shirki kwa dalili ya kauli yake "- na makosa yake yakamzunguka" yani yakamzunguka mwenye kuyatenda, na hayakumwachia njia ya kutokea. Na hili haliwi isipokuwa shirki tu. Kwa maana, yule ambaye ana imani, makosa yake hayamzunguki." Na Al-khawarij waliitumia aya hii kama hoja kwamba mwenye kutenda dhambi ni kafiri. Lakini hiyo ni hoja juu yao kama unavyoona, kwa sababu, inadhihirika waziwazi katika shirki tu. Na vivyo hivyo, mwenye batili anayetumia aya fulani au hadithi sahihi kama hoja yake katika kusema batili (uongo); ni lazima kuna hoja juu yake katika hicho alichotumia kama hoja yake.