انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · البقرة
السورة ٢

البقرة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٧٦

وَإِذَا لَقُوا۟ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ قَالُوٓا۟ ءَامَنَّا وَإِذَا خَلَا بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ قَالُوٓا۟ أَتُحَدِّثُونَهُم بِمَا فَتَحَ ٱللَّهُ عَلَيْكُمْ لِيُحَآجُّوكُم بِهِۦ عِندَ رَبِّكُمْ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ٧٦

(76) Kisha akataja hali ya wanafiki katika Watu wa Kitabu, akasema "Na wanapokutana na wale walioamini, husema: Tumeamini." Basi wakawadhihirishia imani kwa kusema kwa ndimi zao yasiyokuwa katika nyoyo zao. "Na wanapokuwa peke yao, wao kwa wao" bila ya kuwepo pamoja nao yeyote asiyekuwa wa dini yao, wanaambiana wao kwa wao, "Mnawaambia (mambo) aliyokufunulieni Mwenyezi Mungu." Yani mnawadhihirishia imani na kuwaambia kuwa nyinyi ni kama wao? Basi hilo likawa ni hoja yao juu yenu, wakisema kuwa: Hakika wao (Watu wa Kitabu) wamekiri kwamba tuliyo juu yake ni ya haki, na waliyo juu yake ni ya uongo. Basi wakawahoji kwa hilo kwa Mola wenu Mlezi. "Basi hamfahamu nyinyi?" Yani hamna akili, mkaacha lile ambalo ni hoja juu yenu?