البقرة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَظَلَّلْنَا عَلَيْكُمُ ٱلْغَمَامَ وَأَنزَلْنَا عَلَيْكُمُ ٱلْمَنَّ وَٱلسَّلْوَىٰ ۖ كُلُوا۟ مِن طَيِّبَـٰتِ مَا رَزَقْنَـٰكُمْ ۖ وَمَا ظَلَمُونَا وَلَـٰكِن كَانُوٓا۟ أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ ٥٧
(57) "Na tukakutilieni kivuli kwa mawingu na tukakuteremshieni Manna" nalo ni jina linalojumuisha kila riziki [njema] inayopatikana bila ya taabu. Na miongoni mwake ni tangawizi, uyoga, mkate, na mengineyo. "Na Salwa" Naye ni ndege mdogo anayeitwa kware, mwenye nyama nzuri. Na alikuwa akiwateremshia Manna na Salwa (kware) vinavyowatosha na kama riziki ya kuwatunza. "Kuleni vitu vizuri hivi tulivyokuruzukuni." Yani riziki ambayo hawapewi mfano wake watu wa miji mingine waliostareheshwa. Lakini hawakushukuru neema hii, na wakaendelea na ugumu wa nyoyo na wingi wa dhambi. "Nao hawakutudhulumu Sisi." Yani kwa hayo matendo yaliyohalifu maamrisho yetu. Kwa sababu, Mwenyezi Mungu hadhuriwi na uasi wa waasi. Kama vile hakumnufaishi kumtii kwa wenye kutii. "Lakini walikuwa wanazidhulumu nafsi zao." Hivyo madhara yake yakawarudia wao.